Select Menu

ads2

ads2

Habari

Mikasa

Makala

" });

Kimataifa

Burudani/Michezo

Siasa

Julius Nyerere

Ndugu zangu wapendwa.

Nianze kwa kuwashukuru sana kwa ushirikiano ambao mmenipatia toka enzi na enzi nilipoanza kublogi. Hakika najivunia nyie wasomaji na wadau wangu kwani bila nyie, si ajabu ningeshanyoosha mikono zamani sana. Ndio, wapo ambao nilianza nao lakini leo hii hawako hewani tena. 

Safari yangu ambayo ilianza toka mwaka 2005, haijawa safari nyepesi kama ambavyo wengi wanaweza kufikiri. Hakika imekuwa ni safari yenye kila aina ya changamoto. Kuanzia zile za kifikra, kielimu na nyinginezo nyingi, japo zaidi changamoto ya kiteknolojia ndio ilikuwa kubwa zaidi. Hata hivyo, nashukuru kuwa kwa uwezo wake muumba, kwa ule moyo ambao nyie wasomaji na wadau mmekuwa mkinipa, niliweza kuvuka vikwazo mbalimbali hadi hapa nilipo.

Kwa wale ambao tumekuwa pamoja kwa wakati wote huo, nadhani mtakumbuka kuwa nilianza kublogi kwa kutumia jina la msangimdogo, na nilidumu kwa anwani hiyo kwa muda kiasi kabla ya kuhamisha maskani kwenye anwani hii ya sasa ya uchambuzi, ambako nilidumu kwa muda mrefu zaidi. Lengo la kuhama huko, lilikuwa ni katika kuboresha zaidi kazi zangu na lilikuja baada ya kupata ushauri toka kwa wadau mbalimbali ambao walipendelea niachane na jina langu na kuwa na jina ambalo lingemaanisha zaidi kile kilichokuwa kikifanyika katika blogi yangu hii.

Hata hivyo, kwakuwa nimekuwa mtu wa kupokea zaidi ushauri na kuufanyia kazi pale ambapo nilionelea kuwa unafaa, niliendelea kupokea ushauri huo hata baada ya kuwa katika maskani hii. Na miongoni mwa ushauri ambao nilionelea kuwa nilitakiwa kuufanyia kazi zaidi ulikuwa ule wenye kuhusu ubora wa kazi zangu na kuwa nilitakiwa kuwa na maskani kubwa zaidi na yenye hadhi ya kile ninachokifanya. Na ni katika uelekeo huo basi ambapon nilikuja ibuka na Jukwaa Huru Media Inc.

Jukwaa Huru Media Inc. maskani yangu ya sasa (kwakweli sio mpya sana maana wengi washaizoea sasa), ni kampuni rasmi ambayo imelenga katika kuleta mabadiliko makubwa zaidi katika tasnia ya kublogi ndani ya Tanzania na hata nje ya mipaka ya nchi yetu. Huu ni mradi wa habari uliojikita zaidi katika njia ya mtandao, ukiwa na karibu kila kitu chenye kustahili kuwepo katika mradi wowote wa habari.

Ni mradi ambao una channel yake ya TV katika mtandao maarufu wa YouTube, channel yake kwa ajili ya habari katika mfumo wa sauti (Audio) katika mtandao wa Sound Cloud, na ukiwa na ukurasa wake mahususi katika mtandao wa kijamii wa FaceBook pia.

Huku ndiko ambako Msangi Mdogo, anapatikana hivi sasa, huku ndiko ambako Uchambuzi ilikohamia, na huku ndiko ambako kuna kila kitu. Kuanzia kazi zile za zamani ambazo zilipendwa sana kama za Serikali yenye Hang'over ya Mapanki na nyinginezo, hadi mambo mapya ya kisasa zaidi. Kifupi huku ndiko kila kitu na kwa taarifa hii basi, napenda kuwajulisheni kuwa hivi sasa nimehamia katika maskani yangu ya Jukwaa Huru Media Inc (www.jukwaahuru.com) na pia kuchukua fursa hii kuwakaribisha rasmi huko yaliko makazi mapya.

Asanteni sana kwa muda wote ambao mmekuwa mkiniunga mkono kupitia hapa, na naamini mtaendelea kuniunga mkono kwa nguvu, ari na kasi zaidi kupitia Jukwaa Huru Media Inc.

MSANGI, Ramadhani Said
Founder & CEO
Jukwaa Huru Media Inc.
P. O. Box 693, Mbeya
Hotline: +255 713 412176
Email: msangirs@jukwaahuru.com
Website: www.jukwaahuru.com

Waswahili husema atafutaye hachoki, akichoka basi ujue kapata. Bilashaka hiki ndicho kinachoendelea kwa mwanadada Sarah Peter. Bado safari yake ya kuelekea kwenye kitu chenye ubora wa hali ya juu sana ingali inaendelea. Mwanzoni kabisa, mapambano, harakati na mchakato ulianzia katika http://www.angaliabongo.blogspot.com. Kisha akahamishia makazi katika anwani ya http://www.angaliabongo.co.tz/ na baada ya kudumu hapo kwa muda kiasi, leo hii nimepokea ujumbe toka kwake ukisomeka kama ifuatavyo:

Natatumaini kuwa mnaendelea vyema na shughuli za kila siku za kujenga taifa..Jambo la msingi tu kuhusu email hii hi kuwaomba wana blog wenzangu kuweza kunisaidia kuwataarifu wasomaji kupitia blog zenu kuhusu mabadiliko ya blog yangu kutoka www.angaliabongo.co.tz na sasa kuwa www.angalia-bongo.com
Natumaini mtaweza kunisaidia kwa hilo. NATANGULIZA SHUKRANI ZA DHATI.  SARAH.
So, we are officially announcing that, ANGALIA BONGO, is now accessible from  www.angalia-bongo.com 
Kuna mwenye swali hadi hapo? 

Sehemu ya umati wa wakazi wa Mbeya, wakielekea viwanja vya Ruanda Nzovwe, kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Dk Slaa